Advertisement

Responsive Advertisement

Navigation Menu

Radio ni muhimu kuibua vipaji vya watoto nchini .
Kila ifikapo Feb 13, Dunia huadhimisha maashimisho  ya Radio ikiwa nchini Tanzania huadhimishwa makao makuu ya nchi mjini Dodoma.
Maadhimisho hayo yanajumuisha waandishi wa habari  wa vyombo vya habari vya jamii kutoka Tanzania Bara na Visiwani na Wadau wengine wa habari, huku Mgeni Rasmi katika maadhimisho hayo atakuwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mh. Dkt. Harrison Mwakyembe.
Kauli Mbiu ya Redio Jamii mwaka 2018 ni Redio na Michezo huku msisitizo mkubwa ukielekezwa kwenye utandawazi katika suala la kutoa kipaumbele cha kutangaza michezo,  usawa wa kijinsia katika michezo na kutangaza michezo pamoja na kuhuisha amani kupitia michezo.
Redio zimekuwa na mchango mkubwa katika kuibua matatizo yanayowakabiri watoto na kupunguza matatizo hayo pamoja na kuibua vipaji ikiwepo michezo ambayo huwasaidia kujifunza mambo mbalimbali.
  Michezo kwa watoto ni nyenzo ya ujenzi wa jamii bora huku ikiwepo baadhi ya  michezo ya asili (jadi) ambayo watoto wengi hucheza ni kama vile kuruka kamaba, kuimba, rede, komborela, mdako, nage na ukuti.
 Je, ilkiwa leo ndio siku ya radio duniani Watoto wana pewa nafasi gani kushiriki kuwasilisha mawazo yao chanya kwenye jamii yao? Hasa kwenye michezo yao, kugudua  vipaji vyao,kama vile Utangazaji, Uwandishi wa habari na kuviendeleza?

Post a Comment

0 Comments