Advertisement

Responsive Advertisement

Navigation Menu

watoto wachanga zaidi ya watatu hadi wanne wanalazimika kulazwa kwenye kitanda kimoja kwa upungufu wa vitanda kwenye kituo cha afya.February 23, 2018
Kituo  cha  Afya  cha Kibaoni, wilaya ya Kilombero Mkoani Morogoro kinakabiliwa  na  changamoto  ya watoto wachanga zaidi ya watatu hadi wanne kulazwa kwenye kitanda kimoja.
Wakizungumza na Tanzaniakidstime baadhi ya akina mama wamesema kuwa hali hiyo ni changamoto kwao, kwani hulazimika kuwalaza watoto wachanga kwenye kitanda kimoja zaidi ya watatu kutokana na uhaba wa wodi.
Aidha pamoja na changamoto hiyo inayowakabili akina mama hao pindi wanapojifungua  wamesema kuwa, hawana njia mbadala zaidi ya kufanya hivyo  kutokana na huduma hiyo katika kituo cha Afya  Kibaoni  kutolewa  bure.
Mratibu wa Huduma za Afya  ya Uzazi kwa Babaa, Mama na Mtoto Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero Bi Dionisia Danda amekiri Kuwepo kwa changamoto hiyo, inatokana na chumba cha wazazi kuwa kidogo ukilinganisha na idadi kubwa ya wazazi ambao hujifungua katika kituo hicho.
Pia  Bi. Dionisia amesema kuwa, zaidi ya watoto 320 hadi watoto 400 huzaliwa ndani ya mwezi mmoja pekee, hivyo idadi hiyo ya watoto hailingani na uwezo wa wodi hiyo ya wazazi
Hata hivyo amebainisha kwamba, wanamkakati wa kuongeza majengo hususani wodi ya  wazazi ili kuitatua changamoto hiyo.

Post a Comment

0 Comments