Advertisement

Responsive Advertisement

Navigation Menu

watu ambao hukaa na watoto ni vema kuwa makini kwa kuwakumbusha watoto kujisomea .



February 23, 2018.
Wazazi na Walezi wametakiwa kuwahimiza watoto kwenda shuleni ili kujifunza mambo mbalimbali na wakiwapo nyumbani wanapaswa kujisomea mara kwa mara huku wazazi hao wakiwakagua daftari zao mara baada ya kutoka shuleni.
Hayo yameelezwa na baadhi ya wazazi Raphael Mwango na Pius Mwenda mjini Ifakara Mkoani Morogoro wakati wakitoa maoni yao juu ya uhamasishaji wa elimu shuleni kwa watoto wao.
  Aidha wameeleza kwamba,  watu ambao hukaa na watoto ni vema kuwa makini kwa kuwakumbusha watoto kujisomea nyumbani wakati wanapotoka shule ili kuongeza ufaulu wa mwanafunzi katika masomo yake.
Pia wamewataka wazazi na walezi kuwapa uhuru watoto wao katika michezo mbalimbali kwa ajili kuimarisha viungo, kuongeza  ufahamu  ili kujijengea uwezo wa kutambua mambo mbalimbali ikiwa huimalika kimwili na kiakili.

Post a Comment

0 Comments