Advertisement

Responsive Advertisement

Navigation Menu

Wazazi na Walezi Mji mdogo wa Ifakara mkoani morogoro wameshauliwa kuwapeleka Watoto waokwenye masomo ya ziada baada ya kutoka shuleni ilikuwasaidia ufahamu wao.

IFAKARA  FEBRUARY 14, 2018
  Martini  Center ni Kituo cha   masomo ya ziada kilichopo katika Halmashauri ya Mji wa Ifakara mkoani Morogoro  kimewaomba  wazazi, walezi wasiwache watoto nyumbani mara  baada ya kutoka  shuleni  ni vyema kuwapeleka katika vituo vya masoma ya ziada ili watoto wapate muda mrefu wakusoma lengo likiwa ni kufaulu kwakiwango kinacho takiwa kwenye masomo yao.
Akizungumza na Tanzania Kidistime Mwalimu Martini  amesema  hayo baada ya kuona baadhi ya wazazi kuwaacha watoto wanapotoka shule bila kuwatafutia masoma ya ziada ambayo husaidia mwanafunzi kuongeza molali na mazingatio ya masoma pamoja na kupata hali ya kujiamini wakati wote.
 Aidha Martini amesema mwanafunzi  hmijengea hali nzuri ya  kiafya , akili na kuwa na msukumo wa kusoma  kila siku hali ambayo huweza kumuongezea mtoto uelewa zaidi wa masomo yake.
Hata hivyo Mwalimu Olesti Asenga wa Martini Center amewaomba walimu wenzake wafundishe wanafunzi kwa maadili mema na kufuata  mitaala iliyopo na ni bora kutafuta maarifa zaidi juu ya ufundishaji wa watoto  wanapopata muda wa masomo hayo wazingatie masomo yao wakati wote kwani elimu ndio msaada wa maisha yao.

Post a Comment

0 Comments