Advertisement

Responsive Advertisement

Navigation Menu

Wazazi na walezi Manispaa ya Morogoro wameshauriwa kuwalea watoto katika malezi bora kwa kuzingatia misingi na kanuni za Afya.

 Wazazi na walezi Manispaa ya Morogoro wameshauriwa kuwalea watoto katika malezi bora kwa kuzingatia misingi na kanuni za Afya ili kuwaepusha na magonjwa ya lishe duni kama utapiamlo.

Akizungumza na tanzaniakidstime Mwalimu wa shule ya awali ya Ebeneza  Irene Mallya ameeleza kuwa, wazazi na walezi hawazingatii muda maalumu uliopangwa kwenda kuwachukua watoto wao shuleni hapo jambo ambalo hupelekea mtoto kukaa kwa muda mrefu pasipo kupata chakula.

Mwalimu Mallya amesema kwamba, wazazi na walezi wanatakiwa kufuatilia kwa ukaribu, maendeleo ya watoto wanapokuwa katika shule mbalimbali  ili kufahamu mapungufu yaliyopo shuleni hapo, kufuatilia mwenendo wa mwanafunzi na waalimu.

Hata hivyo Mwalimu Mallya amewataka wazazi na walezi wa shule hiyo, kufuata utaratibu wa malipo ya ada kwa watoto hao ili kuongeza hamasa kwa walimu katika utoaji bora wa Elimu.

Post a Comment

0 Comments