Advertisement

Responsive Advertisement

Navigation Menu

Ghouta Mashariki nchini Syria wahangaikazaidi.


  Rais wa Baraza la Usalama kwa mwezi huu wa Machi ni Uholanzi ambapo Waziri wake wa Mambo ya Nje Stef Blok ndiye aliongoza kikao hicho.
Bwana Blok alionyesha picha za watoto wa Syria ambao angalau wao waliweza kukimbia nchi hiyo na sasa wanaishi Uholanzi akisema wao walibahatika.
Alihoji vipi kwa wale waliosalia Syria?
 “Nini mustakhbali wa watoto walio kwenye picha niliyoonyesha. Je siku moja wataweza kurejea Syria. Kama ilivyo kwa watoto wote, nao wanatamani maisha ya kawaida, utulivu na usalama. Mimi mwenyewe ni mzazi na nadhani siko peke yangu kwenye Baraza hili. Picha za watoto walioathirika kwa vita lazima zinamgusa kila mtu. Licha ya tofauti zote baina yetu, angalau tuwe na jambo la pamoja, imani ya kulinda watoto lazima ipatiwe kipaumbele.”
Na ndipo akaweka bayana.
 “Ni wajibu yetu kurejesha uhalali wa baraza hili. Ni juu yetu kuhakikisha kuna mchakato wa kisiasa ambamo kwamo wasyria na wadau wote wanawakilishwa. Na ni wajibu wetu kumaliza chuki na kurejesha utu na ubinadamu kwa wananchi wa Syria.”

Tarehe 15 Machi 2018 familia za eneo la Beit Sawa huko Ghouta Mashariki nchini Syria wakisubiria mabasi ya kuwahamishia maeneo mengine salama huko Hamourieh.
Hali ni mbaya zaidi huko Ghouta Mashariki na Idlib. OCHA inasema kuwa tangu tarehe 9 mwezi huu zaidi ya watu 80,000 wamekimbia Ghouta.Kama hiyo haitoshi, zaidi ya watu elfu 50 wanaishi kwenye makazi duni yaliyojaa kupita kiasi. Taarifa hii ni kwamjibu wa radio ya umoja wa mataifa UN RADIO. 


Post a Comment

0 Comments