Advertisement

Responsive Advertisement

Navigation Menu

Kitengo cha huduma ya mama na mtoto katika Hospitali ya Rufaa Ifakara Mkoani Morogoro kimewataka wanaume na wajawazito kwenda cliniki kila mwezi mara baada ya kugundua mkewe amepata ujauzito.
08 MARCH 2018               IFAKARA                   AFYA
Kitengo cha huduma ya mama na mtoto katika Hospitali ya Rufaa Ifakara Mkoani Morogoro kimewataka wanaume na wajawazito kwenda cliniki kila mwezi mara baada ya kugundua mkewe amepata ujauzito.
Akizungumza na Tanzaniakidstime mmoja wa wahudumu katika kitengo hicho  Hidaya Lyakunga amesema kuwa, lengo ni kupima afya zao na endapo watabainika kuwa na magonjwa mbalimbali ikiwemo Kaswende, na malaria yatadhibitiwa mapema ili kwa kumkinga mtoto.
Aidha Bi. Hidaya amesema mama mjamzito ni vema kuhudhuria kliniki mapema ili kupatiwa elimu ambayo itamsaidi  kuepukana magonjwa ya kuambukizwa pia kutambua kundi lake la damu, pamoja na kujua maeendeleo ya mtoto aliyepo tumboni.
Pia amesema kuwa, wajawazito ambao hawapendi kuhudhulia kliniki wapo katika hatari ya kupatwa na matatizo mbalimbali baada ya kukosa ushauri na elimu juu ya afya wakati wa ujauzito kikiwapo kifafa cha mimba, kuharibikiwa na mimba, kuzaa mtoto mlemavu,  pamoja na kuzaa mtoto akiwa na maambukizi ya magonjwa mbalimbali.

Post a Comment

0 Comments