Advertisement

Responsive Advertisement

Navigation Menu

Miaka 30 jela atakae bainika kubaka au kulawiti mtoto.
        05 FEBR 2018 WIZARA YA AFYA  TANZANIA
  Wizara ya Afya kupitia kitengo cha maendeleo ya jamii jinsia wazee na watoto nchini imesema mikoa inayo ongoza kwa matukio ya ukatili dhidi ya watoto kama vile Ubakaji na Ulawiti nikanda ya pwani ikiwemo Dar es salamu,Tanga,Lindi,Mtwar na  Pwani kwa Tanzania bara huku Tanzania visiwani ikishika nafasi ya kwanza.
  Akizungumza na Okoa Fm Radio kwa mahojiano maalum kupitia kipindi cha Watoto Mkurugenzi msaidizi wa Idara ya Watoto Nd. Benedict Misan amesema idadi ya watoto wanao fanyiwa vitendo vya ukatili kwa sasa inaonyesha kuongezeka jambo ambalo sikweli isipokuwa kwasasa matukio hayo huripotiwa kwahalaka zaidi kwenye vyombo vya habari.
  Hata hivyo amesema kwamba kila mzazi na walezi hawapaswi kumwamini mtu yeyote awe ndugu na wageni wanao tembelea ndani ya familia zao kuwakabidhi watoto wadogo kulala nao chumba kimoja kwani utafiti uliofanywa unaonyesha kwamba walio fanya ukatili huo niwatu wandani  ya  familia.
  Aidha Nd, Misan amebainisha kwamba serikali kupitia wizara ya afya wameweka mpango wamiaka mitano kuzuia ukatili dhidi ya watoto kuanzia mwaka 2017 hadi 2022 ambapo huduma za Uelimishaji na Utoaji wa taarifa kwenye madawati ya jinsia, Nawanao jihusisha na vitendo hivyo maramoja huku yao hutolewa na kutumikia kifungo endapo akibainika na kosahilo.
   Saimoni Zabron yeye ni msimamizi mashauri kutoka kwenye shirika lisilo la kiserikali liitwalo Hacoca linalo pinga ukatili kwa mama na mtoto lililopo mkoani morogoro amesema wanapokea kesi nyingi zaukatili kutoka maeneo mbalimbali yamkoa hasa ikiwemo wilaya ya Mvomero,Morogoro manispaa na Kilosa.

Post a Comment

0 Comments