Advertisement

Responsive Advertisement

Navigation Menu

Nimwaka wa 7 wa mzozo wa Syria umekamilika na sasa mwaka wa 8 umeanza na hakuna nuru ya kumalizika kwa mzozo huo, lakini bado tusikate tamaa, amesema Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres hii leo.

www.tanzaniakidstime.org /https://news.un.org/sw/

Mwaka wa 7 wa mzozo wa Syria umekamilika na sasa mwaka wa 8 umeanza na hakuna nuru ya kumalizika kwa mzozo huo, lakini bado tusikate tamaa, amesema Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres hii leo.
Mwaka wa saba wa vita vya wenyewe kwa wenyewe ukitimia nchini Syria, Katibu Mkuu wa Umoja wa Matifa Antonio Guterres ameelezea machungu yake yanayokumba raia wasio na hatia wakiwemo watoto.
Akihutubia Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lililokutana leo mahsusi kuangazia Syria ambako vita sasa imeanza mwaka wa nane, Katibu Mkuu amesema mwaka 2017 umeshuhudia idadi kubwa zaidi ya watoto wakiuawa, maeneo mengi ya nchi hiyo  yamezingirwa, makombora yanaporomoshwa na usaidizi wa kibinadamu  umekumbwa na sintofahamu kubwa.
Amesema azimio namba 2401 la Baraza la Usalama lililotaka kusitishwa kwa chuki baina ya pande kinzani na sitisho la mapigano kwa siku 30 bado halijaweza kuzaa matunda.Bwana Guterres amesema ingawa kuna maeneo ambako ukali wa mapigano umepungua bado hali si shwari..
 Hasa katika eneo la Ghouta Mashariki, urushaji wa makombora kutoka angani na ardhini umeshika kasi hata baada ya kupitishwa kwa azimio, na imesababisha vifo vya mamia ya raia, ikiripotiwa idadi ni zaidi ya 1,000. tembelea ,https://news.un.org/sw/

Post a Comment

0 Comments