Advertisement

Responsive Advertisement

Navigation Menu

Nigeria yazidi kupokea wakimbizi kutoka cameroon hadi kufikia idadi ya watu 20,000. Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi duniani UNHCR, limeshtushwa na ongezeko la idadi ya wakimbizi wa Cameroon  wanaosaka hifadhi Nigeria ambapo idadi yao sasa imefikia 20,000.
Aikaterini Kitidi ambaye ni msemaji wa UNHCR, mjini Geneva, Uswisi amesema hayo akizungumza na waandishi wa habari   kuwa taarifa kutoka kwa washirika wao ni kwamba zaidia ya asilimia 95 ya wasaka hifadhi wanakosa huduma muhimu kama chakula na malazi.
Amesema baadhi ya familia wamebakiza mlo mmoja kwa siku moja kutokana na upungufu wa chakula.
"Hadi sasa ofisi yetu imekuwa ikifanya  kazi ya kutoa huduma  kwa wakimbizi hawa chini ya mpango wa dharura wa dola 18 milioni. Hata hivyo, hadi sasa hakuna fedha zilizopokelewa, na kusababisha changamoto kubwa na mapungufu katika utoaji huduma."
Na kuhusu ushirikiano baina ya UNHCR na serikali ya Nigeria Bi Kitidi amesema
"Mapema mwezi huu, mamlaka nchini Nigeria ilitenga ardhi kwa UNHCR ambayo inapaswa kuruhusu makazi ya wakimbizi hao ili kuhakikisha usalama wao. UNHCR inaendelea kushirikiana mamlaka husika kususu kuhamishia makazi ya  wakimbizi angalau kilomita 50 kutoka mpakani, kulingana na sheria za kibinadamu."  Hii nikwamjibu wa UNRADIO


Post a Comment

0 Comments