Advertisement

Responsive Advertisement

Navigation Menu

Sudani kusini wagwuzia kilio chao sasa kwa mungu.


  Tangu mwezi disemba mwaka 2013, Sudan K usini imekuwa katika vita vya wenyewe kwa wenyewe. Maelfu ya watu wamekimbilia nchi jirani na wengine wamesaka hifadhi kwenye maeneo mengine ya nchi. Hata hivyo hivi sasa wengine wameamua kurejea na kilio chao sasa ni kwa mwenyezi Mungu.
  Nchini Sudan Kusini msimu wa mvua ukitarajiwa kuanza, baadhi ya wakimbizi wa ndani na hata wale waliokimbilia nchi za jirani wameamua kurudi nyumbani angalau kuendelea na maisha yao.
Hapa ni Kajo Keji, mji ulioko jimbo la Equitoria ya Kati nchini Sudan Kusini. Eneo hilo lilikuwa mahame tangu kuanza kwa mzozo nchini humo mwezi disemba mwaka 2013.Hivi sasa nuru ya amani imewezesha baadhi ya wakimbizi kurejea ili kuendeleza maisha yao na miongoni mwao ni Grace Kobong akikagua lililokuwa shamba lake la mihogo hatahivyo amesema.
 “Napanga kurejea hapa na kuishi. Mwanangu alifariki dunia na sina mtu wa kunisaidia. Alizoea kuja na kunisaidia kuvuna mihogo lakini sasa hayupo. Nimerejea ili nilime na nasaka mbegu za mahindi nipande.”    Kwa taarifa zaidi tembelea https://news.un.org/sw/

Post a Comment

0 Comments