Advertisement

Responsive Advertisement

Navigation Menu

Sudani Kusini njaa yapoteza matumaini kwa wana nchi ambapo watoto ndio wanao teseka zaidi kukabiliana na jangahilo.


Zaidi ya watu milioni saba nchini Sudan kusini sawa na theluthi mbili ya watu wote huenda wakakabiliwa na hali mbaya ya uhakika wa chakula katika miezi michache ijayo kusipopatikana misaada ya kibinadamu.
Onyo hilo limetolewa na shirika la mpango wa chakula duniani WFP ambalo sasa linahaha kupata fedha za kutosha kutoa msaada kwa watu hao nchini SUDANI KUSINI.
Hatahivyo mtoto Nyadane Kuony mwenye umri wa miaka minne hulia wakati anapo hisinjaa Akiwa na babu na bibi yake  waliokimbia vita huko Bentiu mwaka 2016, baba yake alifariki dunia kabla hajazaliwa na mama yake kwa sasa hayupo. Binti huyo alianza matatizo ya utapia mlo vita vilipochachamaa  nchini humo.
Hivi sasa kukiwa na uhaba mkubwa wa chakula watu wamegeukia kula mianzi na matunda mwitu. Mine Pusk Luoch ana umri wa miaka 8 tu amesema"Nimekuja hapa kula mianzi hii kwasababu hatuna chakula.”
  Maelfu ya wakimbizi wa Sudan kusini wanaendelea kumiminika katika nchi jirani ikiwemo Kenya ambako kambi ya Kakuma inahifadhi zaidi wakimbizi 106,000 kutoka sudan kusini. WFP inawapa msaada wa chakula wanapo pokelewa tu kama anavyofafanua Martin Karimi msemaji wa shirika hilo nchini Kenya.
 Tunapokea takribani watu elfu moja kila mwezi, wanapowasili WFP inawapa mlo wa moto kabla hawajapewa vipande vya ardhi ambako wataendelea kupokea mgao wa chakula pamoja na fedha taslim kutoka WFP.”Hivi sasa WFP inatoa chondechonde kwa wahisani na wafadhili kutoa fedha ili kusaidia shirika hilo kuokoa maisha ya maelfu ya wakimbizi hao. Tembelea www.news.un.org

Post a Comment

0 Comments