Advertisement

Responsive Advertisement

Navigation Menu

Uganda imekumbwa na wakimbizi wengi mwaka huu hadi kufikia 60,000 na kuibua changamoto katika utoaji wa misaada ya kibinadamu nchini humo.Kutoka Uganda shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR limesema mmiminiko wa wakimbizi kutoka nchi jirani ya Jamhuri ya Kidemokrasai ya Kongo (DRC), siku hizi umekuwa kinyume kabisa na matarajio , mwaka huu wakimbizi 60,000 wameingia, na kuibua changamoto katika utoaji wa misaada ya kibinadamu kwao. 
Joyce Munyao-Mbithi Afisa Mwandamizi wa Uhusiano wa UNHCR, Uganda amesema kwamba katika siku chache zilizopita, wameanza kupokea wakimbizi Zaidi ya 1,000 kwa siku wakiwa wameangezeka kutoka wakimbizi kati ya 200 na 300 mapema wiki iliopita.
Amefichua kwamba wamepokea takriban elfu tano kabla ya kumaliza hata miezi mitatu ya mwaka huu ambamo walitarajia wakimbizi wasiozidi elfu sitini.
  Hata hivyo ameongeza kuwa wanakabiliwa na changamto za kuwahudumia na kwamba watakabiliwa na kipindi kigumu zadi endapo wahisani hawatajitolea kutoa misaada Zaidi.
Mgogoro wa kikabila Jimboni Ituri na mashambulizi ya vikundi vilivyojihami katika Jimbo la Kivu Kaskazini, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, ndio sababu ya mmiminiko huu wa wakimbizi
Aidha Munayo-mbithi amesema haya wakati UNHCR, na wadau wake wanakumbana na mlipuko wa maradhi ya kipindupindu ambayo kwa sasa yameambukiza wakimbizi Zaidi ya 1,000 wakiwemo 33 waliothibitishwa kufariki dunia.  Taarifa hii ni kwa hisani ya news.un.org/sw

Post a Comment

0 Comments