Advertisement

Responsive Advertisement

Navigation Menu

Unhcr hofu yake inaongezeka kufuatia madhila yanayowakabili wanawake na watoto.

Wakati idadi ya watu wanaokimbia eneo linalozungumza kiingereza nchini Cameroon na kuingia Nigeria ikiongezeka, Shirika la Umoja wa Mataifa la luhudumia wakimbizi UNHCR linasema hofu yake inaongezeka kufuatia madhila yanayowakabili wanawake na watoto.
  Shirika hilo limesema wanawake na watoto ni asilimia 80 ya takribani wakimbizi 10,000 walioorodheshwa Mashariki mwa Nigeria kwenye jimbo la Cross River, huku maelfu ya wakimbizi wengine wa Cameroon katika majimbo mengine bado hawajaandikishwa.
   HatahivyoUNHCR inashirikiana na serikali ya Nigeria kusaidia kuwaunganisha watoto waliotengana na familia zao, kuwapa ulinzi, na kuhakikisha wanapata huduma muhimu. Pia waangalia eneo la kujenga kambi nyingine ambako wakimbizi watahifadhiwa kulingana na viwango vya kimataifa. Taarifa hii nikwamjibu wa UN RADIO.
 

Post a Comment

0 Comments