Advertisement

Responsive Advertisement

Navigation Menu

Watoto zaidi ya 520,000 sasa huenda ikawa zahma kubwa ambapo maelfu ya watoto watakabiliwa na hatari ya magonjwa,na mafuriko.


Usalama na afya ya watoto wakimbizi wa Rohingya zaidi ya laki tano wanaoishi katika kambi zilizo na msongamano mkubwa na makazi yasiyo rasmi nchini Bangladesh iko hatarini hayo yamesemwa na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF.
  Onyo hilo la UNICEF limekuja wakati msimu wa vimbunga na mvua za Monsoon ukijongea nchini Bangladesh , likisema kwamba hali ya kibinadamu ambayo tayari ni mbaya kwa watoto zaidi ya 520,000 sasa huenda ikawa zahma kubwa ambapo maelfu ya watoto watakabiliwa na hatari ya magonjwa, mafuriko, maporomoko ya udongo na pia watoto kutawanywa zaidi.
  Kwa mujibu wa Edouard Beigbeder mwakilishi wa UNICEF Bangladesh amesema  maji yasiyo salama , upungufu wa vifaa vya usafi na mazingira machafu vinaweza kusababisha mlipuko wa kipindupindu na homa ya ini aina ya E, magonjwa ambayo hukatili haraka maisha ya kina mama wajawazito na watoto. Christopher Boulierac ni msemaji wa UNICEF.
  Amesema kuwa msimu huo  wa monsoon pia utaweka hatarini makazi ya wakimbizi, mfumo mzima wa maji, vyoo na miundombinu mingine ambayo inasaidia wakimbizi wa Rohingya zaidi ya 650,000 walioingia Bangladesh tangu Agosti 2017 Taarifa hii nikwa mjibu wa UN RADIO.

Post a Comment

0 Comments