Advertisement

Responsive Advertisement

Navigation Menu

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifan Antonio Guterres atoa neno juu ya afya kwakila mmoja duniani kote.


Unganeni nami kutoa wito wa kila mtu apate huduma ya afya! hayo yamezungumzwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifan Antonio Guterres, kwenye ujumbe wake wa siku ya afya duniani
Wazazi wakiwa na uhakika wa tiba na chanjo kwa watoto wao, nao pia wanaweza kushiriki kwenye shughuli za kujikwamua kiuchumi. Hapa ni Sierra Leone watoto wakipatiwa chanjo dhidi ya Polio,7 Aprili 2018
  Katika siku ya afya duniani hii leo, Umoja wa Mataifa unaendelea kupigia chepuo haki ya msingi ya kila mtu kupata huduma ya afya popote pale alipo. Umaskini unaongezewa kasi kwani watu wanatumia fedha nyingi kwenye matibabu.
 Bwana Guterres anasema WHO ambalo ni shirika la afya ulimwenguni lilianzishwa miaka 70 iliyopita kwa msingi kwamba kupata huduma bora ya afya ni haki ya kila mtu.
Ingawa hivyo anasema hadi leo hii bado watu wanakosa huduma muhimu za afya licha ya kauli mbiu ya afya kwa wote, UHC Taarifa hii nikwamjibu wa UN RAADIO.

Post a Comment

0 Comments