Advertisement

Responsive Advertisement

Navigation Menu

Ni miaka 24 baada ya mauaji ya kimbari nchini Rwanda na bado dunia haijifunza chochote kwa kuzingatia ukatili unaoendelea dhidi ya warohingya."


  Hiyo ni kauli ya Adama Dieng mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu uzuiaji wa mauaji ya kimbari, kufuatia ziara yake huko Bangladesh kunahohifadhiwa maelfu ya waislamu wa kabila la Rohingya kutoka Myanmar,akihojiwa na Idhaa ya Umoja wa Mataifa kuhusu ziara hiyo na mauaji ya warohingya huko kaskazini mwa Myanmar Bwana Dieng amesema…
 “Natumaini kwamba kile nilichokiona Cox Bazar na kile nilichoripoti kwa jumuiya ya kimataifa kwa ujumla kitawafanya watu  wawaamini warohingya. Kwa sababu nilishuhudia janga la kibinadamu ambalo halijawahi kutokea. Ninachosema ni kwamba watu hawa wa kabila ya Rohingya  wanapitia mateso kwa muda mrefu zaidi ambapo wamekuwa wakilazimika kukimbia mauaji katika vijiji vyao na kutembea safari ndefu huku wakivuka mpaka kuelekea Bangladesh, ambako walipokelewa kwa ukarimu .”
Bwana Dieng amesema vyombo vya Umoja wa Mataifa vyenye dhamana ya kukabiliana na changamoto za kiusalama duniani kama Baraza la Usalama, Ofisi ya haki za binadamu na  mahakama ya kimataifa kuhusu mauaji ya kimbari vinapaswa kuzingatia majukumu yao ili kuokoa janga la kibinadamu linalowakumba warohingya huko Myanmar.
 “Kutoridhika kwangu bila shaka, ni kuona kwamba  Baraza la Usalama, chombo ambacho kina jukumu la msingi la kuhakikisha  amani na usalama duniani, hakipo tayari kuzuia uhalifu unaoendela . Tumeona kile kilichotokea Syria. Leo tuna karibu watu nusu milioni ambao wameuawa huko Syria. Tuna karibu watu milioni 7 ambao wapo ukimbizini. Kwa nini tunaendelea kuruhusu hii hali izidi kutokea? Kwa nini tunapaswa kuruhusu matumizi ya silaha za kemikali? Nikiongeza pia mgogoro mwingine, kama ule wa Sudan Kusini.”

 https://news.un.org/sw/story/2018/04/1010501?utm_source=UN+News+-+Kiswahili&utm_campaign=8ee6bd2aee-EMAIL_CAMPAIGN_2018_04_06&utm_medium=email&utm_term=0_36307a21c7-8ee6bd2aee-105232733.

Post a Comment

0 Comments