Advertisement

Responsive Advertisement

Navigation Menu

VIONGOZI WA WHO NA UNICEF WAZUNGUMZIA FAIDA ZA MTOTO KUNYONYA MAZIWA YA MAMA PEKEE
Mtoto anaponyonyeshwa miaka miwili mfululizo bila kupatiwa kimiminika chochote ataepusha gharama kubwa zinazotumika kutibu magonjwa kama vile kuhara, magonjwa ambayo husabaisha na matumizi ya maji yasiyo safi na salama katika kumwandalia maziwa mbadadala badala ya yale ya mama.

Hospitali si tu sehemu ya matibabu bali pia ni pahala ambapo panatakiwa kujenga msingi wa afya bora na hivyo kuokoa vifo, amesema Mkurugenzi Mkuu wa shirika la afya ulimwenguni WHO Dkt. Tedros Ghebreyesus kufuatia uzinduzi wa mwongozo mpya wa shirika hilo na lile la kuhudumia watoto, UNICEF wa kuimarisha unyonyeshaji wa watoto.
Mwongozo huo una hatua 10 zinazolenga ngazi ya kisera hospitali na pia huduma yenyewe ya unyonyeshaji ambapo mashirika hayo yanasema ukizingatiwa utaokoa maisha ya watoto 820,000 kila mwaka wenye umri wa chini ya miaka 5.
Dkt. Tedros amesema katika hospitali nyingi au jamii yoyote ile iwapo mtoto anaweza kunyonyeshwa maziwa ya mama yake au la kunaweza kuleta tofauti kubwa kati ya kifo na uhai. Hii taarifa nikwamjibu wa UN RADIO.

Post a Comment

0 Comments