Advertisement

Responsive Advertisement

Navigation Menu

Who Afrika yasema afya kwa wote nilazima ipatikane ifikapo mwaka 2030.Ili kutimiza ajenda ya kimataifa ya maendeleo yaani SDG’s hapo mwaka 2030 hususani kwa mataifa ya Afrika, basi ni lazima kuhakikisha afya kwa wote inapatikana. Hayo yamesemwa na Profesa Francis Omaswa mkurugenzi mtendaji wa kituo cha afya cha Afrika kwa ajili ya afya ya kimataifa na mabadiliko ya kijamii  nchini Uganda, alieyehudhuria mkutano wa Dunia wa kikanda wa afya uliofanyika mjini Coimbra , Ureno.
  Akizungumza na UN News kandoni mwa mkutano huo Profesa Omaswa amesema kikubwa walichojikita nacho kikubwa , Bi Monica Ferro mkurugenzi wa shirika la Umoja wa Mataifa la idadi ya watu    UNFPA katika ofisi ya Geneva Uswisi amesema amewakilisha shirika lake kwenye mkutando huo ili kujadili umuhimu wa kuwekeza katika afya ya mwanamke
Ni muhimu kuwekeza katika afya yao, ni muhimu kuwekeza katika upatikanaji wa uzazi wa mpango ili kuwapa fursa ya kupanga mwelekeo wa maisha ya baadaye  katika kupata elimu ya kutosha  ili  kuwapa  uwezo na ujasiri wa kuamua maisha yao ya baadaye na pia fursa ya ajira nzuri kama ilivyo kwenye mpango wetu wa kutomuacha  mtu yeyote nyuma.
   Mkutano huo ulioandaliwa na shirika la afya duniani WHO, uliokunja jamvi tarehe 20April mwaka huu na uliwaleta pamoja washiriki zaidi ya 100, mashirika mbalimbali ya Umoja wa Mataifa, asasi za kiraia na wataalamu kutoka Amerika, Ulaya, Asia , Amerika Kusini na Afrika ambayo imewakilishwa na takribani washiriki 100, ili kukuna vichwa na kutoka na mbinu za kuhakikisha lengo la afya kwa wote duniani linatimia. Taarifa hii ni kwa mjibu wa UN Radio.

Post a Comment

0 Comments