Advertisement

Responsive Advertisement

Navigation Menu

Kutegemea msaada ni mtihani kwa elimu ya nchi za kipato cha chini na cha kati:Hali ya kuwa tegemezi wa misaada inadumaza nchi nyingi kiuchumi na hata kijamii, ikiwemo katika maendeleo ya elimu. Sasa nchi masikini na zenye kipato cha wastani zinachagizwa kuondokana na hali hiyo ili kujikwamua na mzunguko wa umasikini ikiwemo elimu duni na jopo la kimataifa la ufadhili kwa ajili ya elimu limezindua ombi la dola bilioni moja kuzisaidia nchi hizo kuepukana na utegemezi.
Changamoto kubwa za elimu zinapatikana katika nchi zenye kipato cha chini na cha wastani na ni kutokana na kuwa tegemezi wa misaada ya wahisani kwa masuala mbalimbali ikiwemo suala la elimu sasa jopo la kamisheni ya ufadhili wa elimu imezindua ombo la dola bilioni moja kuzisaidia nchi hizo. Selina Jerobon na tarifa kamili,Kauli hiyo imetolewa na mmoja wa wajumbe wa jopo la kimataifa la kamisheni ya ufadhili kwa ajili ya elimu Jakaya Mrisho Kikwete.
Akizungumza na Idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa mataifa jijini New York Marekani Rais huyo msataafu wa Tanzania amesema mkakati wa jopo hilo la ufadhili wa elimu ni kuhakikisha nchi nyingi hususani barani Afrika zinatoka katika kipato cha chini cha kutegemea misaada ikiwemo ya elimu na kuingia katika kipato cha wastani jambo ambalo litainua uchumi wa nchi hizo na itakuwa chachu ya kukuza pia kiwango cha elimu hata zikifikiwa kiwango hicho haimaninishi ndio zimeshinda kabisa mtihani. Taarifa hii nikwamjibu wa UN Radio.

Post a Comment

0 Comments