Advertisement

Responsive Advertisement

Navigation Menu

Madereva wa vyombo vya moto Mkoa wa Morogoro wametakiwa kutii sheria pindi wanapoendesha vyombo hivyo ili kuepuka ajali za barabarani hasa kwa watoto.Madereva wa vyombo vya moto Mkoa wa Morogoro wametakiwa kuwa makini kwa kutii sheria pindi wanapo endesha vyombo hivyo ili kuepuka ajali za barabarani.
Akizungumzia changamoto hiyo Ofisa wa kitengo cha elimu kutoka Jeshi la Polisi mkoani Morogoro kopro BATHROMEO NYAMBARI amesema kuwa, ajali nyingi zinazotokea hutokana na madereva kuwa wazembe na baadhi yao kukosa elimu ya usalama barabarani.

Aidha  KOPRO NYAMBARI ameongeza kuwa, bado wanaendelea kutoa elimu mbalimbali kuhusu usalama barabarani kupitia vyombo vya habari, semina kwa madereva hao na shuleni ili wanafunzi watambue namna ya kujiepusha na kujikinga na ajali hizo.
Hata hivyo KOPRO NYAMBARI amewataka Madereva wote nchini, kuwa makini pindi wanapo endesha vyombo vya moto ili kuepusha ajali zisizo za lazima.

Post a Comment

0 Comments