Advertisement

Responsive Advertisement

Navigation Menu

Baada ya kuporwa utoto wao na vita, sasa maelfu ya watoto waishia ukimbizini nchini Uganda.
Wahudumu wa mashirika ya misaada ya kibinadamu nchini Uganda wakiwemo wa Umoja wa Mataifa wanakumbana na changamoto kubwa ya kuwasaidia watoto wakimbizi zaidi ya 250,000 waliotengana na wazazi ama walezi wao kutokana na vita na kusaka hifadhi wakiwa peke yao nchini humo. Mwandishi wa UN nchini Uganda  John Kibego ametembelea makazi ya wakimbizi ya Imvepi Wialayani Arua nchini humo ambako kuna asilimia kubwa ya watoto  na kuandaa tarifa hii.
Wengi wa watoto hao wamekimbia vita nchini Sudan Kusini na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, DRC, miongoni mwao ni mtoto Norman Suku Denis anayesimulia kilichomfanya kufungasha virago
 “Wakati mapigano yalipoanza, mama yangu alimwambia baba yangu tukimbie lakini baba akasema yeye hawezi kukimbia. Tulianza kukimbia na mama yetu lakini aliporudi nyumbani kidogo, alikuta tayari baba yetu ameshauauwa kw akupigwa risasi. Naye mama yangu walimuua”
“Tulianza kukimbia na tukakukuta na watu amabo pia walikuwa wakikimbia kwenda mpakani. Tulikuja nao na kukuta msichana mmoja ambaye tulikuja naye mpaka hapa, walitupatia nyumba na hadi sasa ndiye anatulea”
Norman Suku Denis ambaye sasa ana umri wa miaka 17 na ndugu zake wadogo wawili ni sehemu ndogo tu ya watoto zaidi ya 250,00 walio ukimbizini nchini Uganda.Afisa wa Mawasiliano wa Shirika la Umoja wa Mataifa ya Kuhudumia wakimbizi, UNHCR, Uganda ni Duniya Aslam Khan,Anasema watoto hao wako hatarini bila makuzi stahiki hivyo.
 “Hua tunatabaini familia ambazo zinaweza kutoa huduma ya malezi, nasi kama UNHCR na wadau wetu tunatoa msaada kwa familia hizo. Hii ni changamoto kubwa amabyo haiwezi kushughulikiwa na shirika moja pekee. Tunaomba wahisani kujitolea na kuwekeza zaidi katika ulinzi wa watoto ili tuwe na kizazi salama”
Hata hivyo UNHCR Uaganda inakabiliwa na mtihani mkubwa wa ufadhili hasa wakati huu ambapo wimbi la wakimbizi wanaomiminika nchini humo linaongezeka kila uchao kinyume na matarajio ya shirika hilo. Taarifa hii nikwa mjibu wa radio washirika UN RADIO.

Post a Comment

0 Comments