Advertisement

Responsive Advertisement

Navigation Menu

Chanjo ya kunusuru watoto dhidi ya kuhara yazinduliwa Uganda.

Chanjo itakayo wakinga watoto wa chini ya umli wa miaka mitano na virusi vinavyosababisha kuhara (rotavirus) imezinduliwa nchini Uganda kwa ushirikiano wa serikali na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF.
  Chanjo hiyo iliyozinduliwa rasmi Jumatatu katika wilaya ya Buikwe, itatolewa bure kwenye vituo vyote vya afya nchini Uganda na inatarajiwa kuokoa maisha ya maefu ya watoto wanaofariki Dunia kila mwaka kutokana na ugonjwa wa kuhara.
Mwakilishi wa UNICEF, nchini Uganda Dokta Doreen Mulenga, ameipongeza seriali ya Uganda kwa kujumisha chanjo ya rotavirus katika mpango wa chango wa kitaifa na kusema ni hatua muafaka katika juhudi za kutimiza lengo la afya bora kwa watoto wote, Taarifa hii nikwamjibu wa Radio ya Umoja wa Mataifa UN RADIO. 

Post a Comment

0 Comments