Advertisement

Responsive Advertisement

Navigation Menu

G7:Kuchangia dola bilioni 3 kwa ajili ya elimu ya wasichana.Canada imesema ina mipango ya kuchangia kiasi cha pauni bilioni 2.9 ikisaidiwa na nchi washirika wa G7 kwa ajili ya kusaidia elimu ya wasichana na wanawake walio masikini
Fedha hizo zitasaidia kuhakikisha kuwa mpango wa wasichana na wanawake kupata elimu sawa na wavulana na kuwezesha fursa za kujifunza katika nchi mbalimbali duniani, Serikali ya nchi hiyo imeeleza.
Tangazo hili la siku ya Jumamosi limekuja kwa kuchelewa kwa kuwa nchi washirika wakiwemo Ujerumani,Japan, Uingereza, Umoja wa Ulaya na Benki ya dunia zilikuwa zikiendelea kuchangia
Mkutano wa G7 uliofanyika Quebec ni mkutano wa mwaka unaokutanisha nchi za Canada, Marekani, Uingereza, Ufaransa, Italia, Japan na Ujerumani.
Changamoto ya elimu inayowakabili wasichana duniani
Serikali ya Canada imesema kujitoa kwa ajili ya kuchangia elimu kunawakilisha ''uwekezaji mmoja mkubwa katika elimu kwa ajili ya wanawake na wasichana wanaokuwa katika mazingira yenye changamoto kadha wa kadha''.
Uwekezaji huu unaelezwa kuwa utaweza kuwasaidia watoto na vijana wadogo zaidi ya milioni nane.
Mshindi wa tuzo ya amani ya Nobel Malala Yousafzai, 20 ameunga mkono zoezi hilo la uchangaji fedha.

Post a Comment

0 Comments