Advertisement

Responsive Advertisement

Navigation Menu

Kipaji cha mwanao ni kwa ajili yake na jamii yake


Unaposaidia kuendeleza kipaji cha mwanao faida zake si kwake peke yake bali pia kwa jamii nzima. Huo ndio wito uliojitokeza katika warsha ya siku tatu iliyokutanisha wazazi, walimu na wanafunzi mkoani Pwani nchini Tanzania kwa lengo la kutambua, kuendeleza na kufaidi na vipaji vya watoto hususani yatima na wasiojiweza.
Watoto yatima au wanaoishi katika mazingira ya umasikini nchini Tanzania  mara nyingi hukosa fursa za maendeleo kielimu hata  kimaisha kwa sababu ya kutokuwa na ujuzi wowote limesema shirika lisilo la kiserikali la COMPASSION ambalo ni la kidini  linalowasaidia watoto na vijana yatima katika kusongesha mbele ajenda ya maendeleo endelevu SDG’s.
Shirika hilo linashirikiana na shule mbalimbali za mkoa wa Pwanni hasa zinazotoa elimu kwa watoto yatima na masikini wasiojiweza kupata ujuzi wa kuweza kujitegemea hapo baadaye.
Leo limekamilisha warsha ya siku tatu iliyokutanisha washiriki zaidi ya 300 , walimu na wanafunzi kujadili jinsi ya kutambua, kuendeleza na kufaidika na vipaji walivyonavyo  lakini pia kuichagiza jamii kusaidia kuendeleza vipaji vya watoto wao kwa ajili ya mustakhbali wao. Mwanafunzi Rehema Egidi ni miongoni mwa washiriki

Watoto yatima na watoto kutoka familia masikini wakihudhuria warsha ya siku tatu mjini Kibaha mkoani Pwani nchini tanzania, ya kjinsi gani ya kubaini , kuendeleza na kufaidika na vipaji vya watoto hawa katika shule mbalimbali, ikiwa ni sehemu ya SDG's
(REHEMA EGIDI)
Peter George ni mwalimu wa kazi za mikono
(SAUTI YA PETER GEORGE)
Baada ya siku tatu za warsh watoto  wameambulia nini? Sarafina Alex ni mwanafunzi
(SAUTI YA SARAFINA ALEX)

Post a Comment

0 Comments