Advertisement

Responsive Advertisement

Navigation Menu

Mapigano Afghanistan yawaengua mamilioni ya watoto shuleni Afghanistan.
Mustakhbali wa watoto Afghanistan mashakani kutokana na mapiganoTakribani nusu ya watoto wenye umri wa kati ya miaka 7 hadi 17 nchini Afghanistan hawako shuleni.
Hii ni kwa mujibu wa ripoti mpya ya shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF iliyotolewa ikiangazia watoto wasio shuleni ikijikita zaidi nchini Afghanistan.Sababu kuu zinatajwa ni mzozo unaoendelea nchini humo sambamba na umaskini na ubaguzi dhidi ya watoto wa kike.
Watoto hao milioni 3.7 wasio shuleni ni kiwango cha cha juu zaidi kuwahi kufikiwa nchini        
     Afghanistan tangu mwaka 2002, imesema ripoti hiyo.Asilimia 60 ya watoto hao ni watoto wa kike, hali ambayo ripoti hiyo imesema inawaweka katika hali mbaya zaidi kwa kuzingatia ubaguzi na ukatili mwingine wanaokabiliana nao kutokana na jinsia yao ikiwemo ndoa katika umri mdogo.
Majimbo ambamo kwayo watoto wa kike wana hali mbaya zaidi kielimu ni Kandahar, Helmand, Wardak, Paktika, Zabul na Uruzgan.Akizungumzia ripoti hiyo, mwakilishi wa UNICEF nchini   
      Afghanistan, Adele Khodr amesema kuendelea kuchukua hatua za kawaida hakutaleta manufaa yoyote iwapo jamii ya kimataifa inataka kuhakikisha kila mtoto anapata haki ya elimu. Hii nikwa mjibu wa UN Radio .

Post a Comment

0 Comments