Advertisement

Responsive Advertisement

Navigation Menu

Wajibu wa kulinda ni muhimu sasa kuliko wakati mwingine wowote Watoto wanahali gani kwenye nchi hizo?:Guterres

Majadiliano kuhusu wajibu wa kulinda maisha ya watu ni muhimu sana leo hii kuliko wakati mwingine wowote, wakati dunia ikijitahidi kwa pamoja kuwalinda watu  hao dhidi ya  mauaji ya kimbari, uhalifu wa vita, mauaji ya kikabila na uhalifu dhidi ya ubinadamu.
 Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres hii leo akizungumza katika mjadala wa wazi wa Baraza kuu la Umoja wa Mataifa mjini New York Marekani kuhusu wajibu wa kulinda maisha ya watu , uliopitishwa kwa kauli moja na viongozi wa dunia mwaka 2005 baada ya kushuhudia mauaji ya kimbari ya Rwanda na Sebrenica. Lengo likiwa bayana amesema kuongeza juhudi kwa pamoja kama jumuiya ya kimataifa kuwalinda watu hao.
 “Hata hivyo leo hii bado kuna hofu kwamba kanuni hiyo inaweza kutumika kuchukua hatua ya pamoja kwa madhumuni mengine kuliko yale yaliyoafikiwa katika matokeo ya mkutano wa dunia. Pia kuna wasiwasi juu ya viwango vya pande mbili na matumizi ya kuchagua ya kanuni hizo katika siku za nyuma.”
Na hii ndio sababu amesema uwazi katika kujadili suala hili ni lazima, ili  kuondokana na hisia zisizo sahihi  na kutoaminiana akihimiza “Tunapaswa kuunda uelewa wa pamoja na kutoa msaada mkubwa kwa wajibu huu, kama chombo muhimu cha ulinzi na kuzuia maafa.” Taarifa hii nikwamjibu wa radio ya umoja wa mataifa UN RADIO.

Post a Comment

0 Comments