Advertisement

Responsive Advertisement

Navigation Menu

Bank ya Dunia yatoa riport kuhusu Matrilioni ya Dola yanayopotea kwa kutomsomesha mtoto wa kike


Nchi nyingi duniani hususan zile za kipato cha chini bado zinaona si mtaji kumpeleka shule mtoto wa kike, jambo ambalo hii leo Benki ya Dunia inasema limepitwa na wakati, kwa kuwa ukiwekeza kwa mtoto wa kike umewekeza kwa dunia nzima.
 Fursa finyu za elimu kwa watoto wa kike pamoja na vikwazo vya kumaliza miaka 12 ya elimu husababisha nchi husika kupoteza kati ya a dola trilioni 15 hadi trilioni 30 ambazo zingalichangiwa na watoto hao kupitia nguvu kazi katika jamii zao,Hiyo ni kwa mujibu wa ripoti mpya ya Benki ya Dunia iliyotolewa kuelekea siku ya Malala mapema wiki hii.
Ikipatiwa jina la Fursa zilizopotezwa- Gharama ya kutompeleka shule mtoto wa Kike, ripoti hiyo inasema hali ni mbaya zaidi kwa nchi za kipato cha chini ambako watoto wa kike wanaohudhuria shule ni chini ya theluthi mbili.
Hatahivyo Riport hiyo imebainisha kwamba, wanaojiunga na shule ya sekondari ya awali ni mmoja tu kati ya watatu ambaye anahitimu masomo hayo Taarifa hii nikwamjibu wa Radio Wshirika UN RADIO.

Post a Comment

0 Comments