Advertisement

Responsive Advertisement

Navigation Menu

Dkt.Ndugulile azindua mpango wa mafunzo kwa wanafunzi na walimu ili kupambana na vitendo vya ukatili wa jinsia shuleni.


Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, JInsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile amezindua mpango wa mafunzo kwa wanafunzi na walimu ili kupambana na vitendo vya ukatili wa jinsia shuleni.
Akizungumza katika uzunduzi wa mafunzo hayo uliofanyika katika Shule ya Sekondari Mwisenge Dkt. Ndugulile amesema kuwa vitendo vya Ukatili wakijinsia hususani ukatili dhidi ya wanawake na watoto umeendelea kuwepo chini na takwimu zikionesha mkoa wa Mara ukiwa na asilimia 32 ya vitendo hivyo.
Ameongeza kuwa mimba na ndoa za utotoni bado ni tatizo kubwa ambapo mkoa wa Mara ni wa tano kitaifa kwa kuwa na asilimia 37.
“Serikali imeeandaa Mpango wa kazi wa Kitaifa wa Kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto wa mwaka 2017/18-2021/22 na moja kati ya msisitizo katika mpango huu ni kutokomeza ukatili wa kijinsia shuleni” alisisitiza Dkt. Ndugulile
Aidha Dkt. Ndugulile amekemea mahusiano ya kingono yaliyopo baina ya walimu na wanafunzi na kuwataka wanafunzi kuacha kufanyiana vitendo vya ukatili na kutoa taarifa ya vitendo vya ukatili.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Musoma Bw.Vicent Naano amesema kuwa wataendelea kupambana na wale wote waatakaosababisha au kuwafanyia wanawake na watoto vitendo vya ukatili. Pia Mwakilishi wa Mkurugenzi wa USAID.
 Ameihakiishia Serikali ya Tanzania kuendeleoa kushirikiana nayo katika mapambano dhidi ya ukatili dhidi ya wanawake na watoto na mimba na ndoa za utotoni.
Mpango huu wa mafunzo kwa walimu na wanafunzi utawafikia walimu 1,300 na wanafunzi 26,000

Post a Comment

0 Comments