Advertisement

Responsive Advertisement

Navigation Menu

Naibu waziri atoa tamko kali mkoani Tabora kwa utoro wa wanafunzi katika shule zote za msingi na sekondari.Wananchi mkoani Tabora wametakiwa kutowashirikisha watoto katika jambo lolote litakalo gharimu muda wao wamasomo ili kuhakikisha kilamtoto anapata haki yake ya kikatiba ya kupata elimu itakayomjengea msingi mzuri wa kimaisha.
Hayo yameelezwa leo na Naibu waziri ofisi ya rais tawala za mikoa na serikali za mitaa-TAMISEMI  JOSEPH KAKUNDA wakati wa maandamano ya amani mkoani hapa yakupinga utoro wa watoto shuleni na utumikishwaji wawatoto yaliyofanyika kuanzia sanamu ya mwl.Nyerere hadi ofisi za mkuu wa mkoa yakiwa na lengo la kuhamasisha jamii kupinga vitendo hivyo.
  Aidha Kwaupande wake mkuu wa mkoa wa Tabora AGREY MWANRImuandaaji na msimamizi wa kampeni hiyo amewaonya watoto kutoonekana katika maeneo hatarishi ambapo pia amewataka wananchi na viongozi kutotumia vitendo vya rushwa wakati wazoezi hilo endelevu na kusemakuwa mzazi yeyote atakaye tii amri kwa hiari kuanzia sasa hatahusishwa katika adhabu zilizopangwa.
   Hata hivyo mwanasheria mkuu wa mkoa wa Tabora RICHARD RUGOMELA ametolea ufafanuzi wakisheria juu ya zoezi hilo ambapo ameeleza maamlaka aliyonayo kiongozi husika katika kutekeleza amri aliyoisimamia kwa mujibu wa katiba ya jamuhuri ya muungano wa Tanzania.
   Kampeni hiyo ya kupinga utoro wa watoto shuleni na utumikishwaji wa watoto iliyo na  kaulimbiu isemayo kamata weka ndani kwakutotii amri halali ikisimamiwa na mkuu wa mkoa wa Tabora inalenga kuinua kiwango cha elimu mkoani hapakwa kukomesha utoro wa wanafunzi shuleni, ambapo mkoa wa Tabora inajumla ya wanafunzi  watoro  11004 katika shule zote za msingi na sekondari.

Post a Comment

0 Comments