Advertisement

Responsive Advertisement

Navigation Menu

wasichana wajawazito Burundi wapata changamoto Baadhi ya watoto wakicheza, Burundi
Mashirika ya haki za binadamu yamekosoa hatua ya Burundi ya kuwapiga marufuku wasichana wajawazito na wavulana waliowapa ujauzito huo kurudi shuleni, yakisema hatua hiyo ni ukiukaji dhidi wa haki za elimu kwa watoto.
Mashirika hayo pia yanasema kuwa hatua hiyo ni ubaguzi dhidi ya mtoto wa kike. Juma lililopita serikali ya Burundi ilitoa agizo kwa serikali za mikoa ikisema kuwa wasichana wajawazito pamoja na wavulana waliosababisha ujaouzito huo hawana haki ya kuwa sehemu ya mfumo wa elimu nchini humo.
Katika barua ilioandikwa Juni 26 kwa wakurugenzi wote wa elimu mikoani, waziri wa elimu Janvière Ndirahisha alisema hata hivyo kuwa wanafunzi hao wataruhusiwa kuhudhuria mafunzo ya kiufundi na kozi za kitaaluma.
Agizo ni la ubaguzi 
Lakini makundi ya kutetea haki za binadamu yanasema kuwa kuwazuia watoto kuhudhuria masomo kutakuwa na athari mbaya kwa elimu yao kwenye taifa ambalo asilimia 11 ya wasichana kati ya umri wa miaka 15-19 wanajihusisha na vitendo vya ngono. Takwimu hizo ni kwa mujibu wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia idadi ya watu.
Baadhi ya watoto wakicheza, Burundi
Marufuku hiyo ya taifa hilo la Afrika Mashariki, inalenga kuwazuia wasichana zaidi ya watoto wa kiume, wanasema wanaharakati wakiongoza kuwa ni rahisi kugundua kuwa mtoto wa kike ni mja mzito, lakini ni vigumu kutambua aliyempa mimba.
Wakili wa kikundi kinachopigana dhidi ya marufuku hiyo Naitore Nyamu-Mathenge, anasema marufuku hiyo inamnyima mtoto wa kike elimu pamoja na kuegemea zaidi upande wake.
Anauliza, "serikali inapanga kuthibitisha vipi kuwa mvulana fulani ndiye msichana fulani mimba, na je itakuaje kwa visa ambavyo walimu na watu wazima katika jamii wamehusika, je serikali itawachukulia hatua pia?"

Post a Comment

2 Comments

 1. Nilikuwa nahitaji kufanya kazi na poja na ninyi jinsi zaidi ya kupambambana na ubakaji wa watoto nchin
  tanzania

  ReplyDelete
  Replies
  1. Karibu sana Frida. Ntafurahi kuwasiliana na mimi tumia pia whatasApp no. +255767085647/ Email:tanzaniakidstime2018@gmail.com

   Delete