Advertisement

Responsive Advertisement

Navigation Menu

Watoto wetu, tunu yetu tuwape elimu inayostahili.


Wiki ya elimu Tanzania inaadhimisha juma hili ikibeba kauli mbiu “uwajibikaji wa pamoja katika kutoa elimu bora, watoto wetu tunu yetu”, madhumini ni kuchagiza ufikiaji wa lengo namba 4 la maendeleo endelevu SDG’s lihusulo elimu.
Maadhimisho haya ya wiki ya elimu yaliyoanza Julai 16 na yatakamilika Julai 20 na yanafanyika nchi nzima yakishirikisha pia wadau mbalimbali wa elimu  yakiwemo mashirika ya kitaifa na kimataifa yanayosaidia kusongesha ajenda ya elimu kama shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF na shirika la elimu, sayansi na utamaduni UNESCO.
  Mkoani Morogoro Mashariki mwa nchi hiyo John Kabambala kutoka Radio washirika Tanzaniakids FM ametembelea  maonyesho ya wiki ya elimu  ya mradi wa elimu ya awali unaoendeshwa na shirika la Childhood Development (CDO)  kwa msaada shirika la Children in the cross Fire kutoka Ireland.
Mradi huo ni wa elimu kwa njia ya michezo kwa kutumia vitu vya asili kama mawe, visoda, chupa na vitabu vya picha na unashirikisha shule zaidi ya 40 mkoani humo na Kabambala amemuuliza afisa mradi Joseph Machira kwa nini wameanzisha mradi huo nae amesema kwasababu kuna changamoto kubwa kwenye darasa la awali .

Post a Comment

4 Comments

  1. Integrated school readiness program ISRP in Swahili Watoto Wetu Tunu Yetu ni mradi unaolenga kuweka utayari wa mtoto kaingia darasa la kwanza mradi unalenga sana watoto kuanzia miaka 0-6 hasa wale walio darasa la awali, mradi unakenga kuboresha mbinu za ufundishaji wa darasa la awali kupitia michezo, mradi unasisitiza utumiaji wa zana za asili mfano chupa za Maji, magunzi, vizibo,visoda n.k pia tunasisitiza madarasa changamshi kwa darasa la awali pamoja na lishe mashuleni...Kwa pamoja tutayaboresha madarasa yetu ya awali

    ReplyDelete
  2. Uboreshaji wa Elimu ya awali ni kichocheo kikubwa sana katika ukuaji na Maendeleo ya watoto kwa kujenga utayari wao. Ushirikiano wa pamoja utajenga msingi wa watoto wetu. Karibuni sana tujifunze Elimu ya awali na manufaa yake kwenye Mradi wa Watoto Wetu Tunu Yetu Wilaya ya Mvomero kata za Mtibwa,Doma na Malali kwenye shule za msingi za Serikali zote pia Wilaya ya Kilombero Kata za Mwaya,Mchommbe na Ching'anda. Wekeza sasa kwenye elimu ya awali ya malezi makuzi na mendeleo ya watoto.

    ReplyDelete
  3. Shukrani sana Mr. Peter kwa ujumbe huo mzuri na kwamaoni yako karibu sana.

    ReplyDelete