Advertisement

Responsive Advertisement

Navigation Menu

furaha ya mwanafunzi ni kusomea akiwa ndani ya darasa.

Zaidi ya watoto 500 wa mji wa Yambio katika jimbo la Gbudue nchini Sudan Kusini ambao awali walikuwa wanasomea chini ya miti sasa mwelekeo wao wa elimu umenyooka baada kufunguliwa kwa jengo jipya lenye vyumba vinne vya madarasa.
Jengo hilo la shule ya chekechea na ya msingi ya United, kwa kiingereza United Nursery and Primary Schoo, limejengwa na ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini Sudan Kusini UNMISS  kupitia mradi wa kuleta matokeo ya haraka, au Quick Impact.
Lucy Samuel ambaye ni  mmoja wa wanafunzi wa darasa la nne katika shule hiyo  amesema amejawa na furaha kwa sababu wamejengewa shule nzuri ya wao kujifunzia.
Taarifa ya UNMISS imesema shule hii ilianza mwaka jana ikiwa na wanafunzi 180 wakisomea chini ya miti ambapo hivi sasa imepiga hatua na idadi ya watoto wanaojiunga kutaka kusoma ikiongezeka hadi kufikia zaidi ya watoto 500 Taarifa hii ni kwamjibu wa radio washirika UN radio.

Post a Comment

0 Comments