Advertisement

Responsive Advertisement

Navigation Menu

Idadi ya unyonyeshaji maziwa ya mwanzo mkoani morogoro bado nichangamoto.Wazazi mkoani Morogoro wametakikiwa kuwanyonyesha watoto wao kuanzia miaka sifuri hadi miaka miwili ili  kuwakinga na magonywa yatokanayo na lishe duni.
Akizungumza na Tanzaniakidstime Afisa Lishe wa kituo cha Afya cha sabasaba Mkoani Morogoro ESTER KAWISHE amesema kuwa ,maziwa ya mama humkinga mtoto dhidi ya magonjwa ukiwemo Utapiamlo, ikiwa maziwa hayo yanavirutubisho vyote ambavyo mtoto huhitaji.
Pia Afisa Lishe ESTER, ametoa wito kwa wazazi wa kiume kuwa karibu na kinamama kwa kuwasaidia kutekeleza unyonyeshaji wa maziwa ya mama kwa mtoto.
Kwa upande wake mmoja wa akinamama wanao nyonyesha mtoto Bi. CHRISTINA SEVELIN amesema     kuwa, baadhi ya kinamama huanza kuwapa vyakula watoto  kabla ya wakati, kwa kisingizio  cha kutotosheleza maziwa kwa mama mzazi.
Hata hivyo wakati ulimwengu ukiadhimisha wiki ya kimataifa ya kunyonyesha mtoto na kuelezea faida zake kwa wazazi na taifa, wakazi wa dunia wanahamashishwa kufahamu umuhimu wa maziwa ya mwanzo kabisa ya mama kwa mtoto .
Takriban 40% tu ya watoto wachanga wenye umri kati ya miezi 0 hadi 6 ndio wanaoishi kwa kunyonyeshwa pekee, kwamjibu wa shirika la Afya duniani WHO.

Post a Comment

0 Comments