Advertisement

Responsive Advertisement

Navigation Menu

Jeshi la polsi mkoa wa Morogoro linawashikilia wanawake wawili kwa kosa la kuwafanyia ukatili watoto wao.


Jeshi la polsi mkoa wa Morogoro linawashikilia wanawake wawili kwa kosa la kuwafanyia ukatili watoto wao likiwemo tukiuo la mtoto kupigwa na kuingiziwa mwiko sehemu zake za siri katika kata ya KIHONDA.
Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake kamanda wa polisi mkoa wa Morogoro kamishna msaidizi mwandamizi wa polisi WILBROAD MUTWAFUNGWA amemtaja NAOMI JUMA ambaye ni mama mdogo wa  mototo wa miaka sita  aliyekatiliwa na kuingiziwa mwiko sehemu za siri katika kata ya KIHONDA Manispaa ya Morogoro.
  RPC MUTWAFUNGWA pia amethibitisha kukamatwa  mwanamke  mmoja kwa kosa la kumwadhibu kwa kumchapa fimbo mototo wake mwenye miaka 11na kumsababishia kifo wilayani GAIRO.
Mutafungwa amesema mtoto huyo  ambaye jina lake limehifadhiwa alikua mwanafunzi wa darasa la nne katika shule ya msingi GAIRO.
Katika hatua nyingine kamanda MUTAFUNGWA amekiri jeshi la polisi kuendelea kuchunguza tukio la mhalifun aliyemuiba mototo wa Bi RAHELI STANFOD
katika eneo la kituo cha  mabasi cha mkoa Msamvu.
MUTAFUNGWA ametoa tahadhari kwa wazazi kuwachunga vyema watoto wao na kutowaamini mapema watu hususani wasiowafahamuPost a Comment

0 Comments