Advertisement

Responsive Advertisement

Navigation Menu

mtoto mkimbizi aonyesha hisiazake baada ya kulejea darasani tena.


Mahema hayo  yaliyosimikwa kwenye kambi ya Mabrouka iliyoko katikati mwa  jangwa huko kaskazini-mashariki mwa Syria yanafuatia msaada wa kibinadamu kutoka shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF kwa ushirikiano na wadau wake.
Wavuti maalum unaochapisha habari za watoto wa Syria umemnukuu Joumana ambaye ni mmoja wa watoto walioshindwa kupata elimu ipasavyo kutokana na hamahama na ukosefu wa maeneo ya kujifunzia tangu  mwaka 2012 walipokimbia kijiji chao.
“Kwa miaka kadhaa kipaumbele chetu kimekuwa ni kuishi,” amesema Joumana ambaye kabla ya kujengewa mahema matano ya shule walilazimika kutumia hema moja tu ambalo halikuwa rafiki kwa kujifunzia.
Elimu inayotolewa kupitia mahema haya matano, ni ya kumwezesha mtoto kujifunza mwenyewe ikilenga zaidi watoto waliokosa masomo kwa muda mrefu kama vile Joumana.
UNICEF inasema wafanyakazi wa kujitolea wanashirikiana na watoto hawa ambapo hadi sasa watoto 3,000 kwenye kambi ya Mabrouka wamenufaika.
Joumana anasema, “sikuamini kabisa mwanzoni, wala sikuweza kupata picha mimi niko darasani.”
Tayari Joumana alifanya mtihani wa awali na kupangiwa kujiungana darasa la 6 akisema kuwa “shule haitufundishi tu masomo bali pia tabia na mbinu za mawasiliano na kujenga upya jamii zetu.”
Vita vya wenyewe kwa wenyewe vilianza nchini Syria mwezi Machi mwaka 2011 na hadi sasa hakuna mwelekeo wowote wa kumalizika huku watoto wakisalia kuwa wakimbizi wa ndani na nje ya nchi yao,Taarifa hii nikwa mjibu radio washirika UN radio kwa maelezo zaidi tembelea https://news.un.org/sw

Post a Comment

0 Comments