Advertisement

Responsive Advertisement

Navigation Menu

Ukatili dhidi ya watoto ni lazima ukomeshwe mara moja duniani kote hasa yemen.

Ukatili dhidi ya watoto ni lazima ukomeshwe mara moja, hakuna visingizio tena. Wito huo umetolewa leo na mkurugenzi wa kanda ya Mashariki ya Kati na Afrika Kaskazini wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF.
Geert Cappelaere ametoa wito huo kufuatia shambulizi la anga lililotokea leo nchini Yemen na kukatili maisha ya watoto wengi na wengine kujeruhiwa katika mjini wa Sa’ada Kaskazini mwa Yemen.
Cappelaerre amesema shambulio hilo dhidi ya basi lililokuwa na wanafunzi ni la kusikitisha na kuhuzunisha , na watoto wote hao wamearifiwa kuwa na umri wa chini ya miaka 15 huku duru zikisema makumi ya watoto wameuawa katika shambulio hizo.
Akisistiza umuhimu wa kukomesha ukatili dhidi ya watoto amehoji “kweli dunia inataka kupotea zaidi kwa maisha ya watoto wasio na hatia ndio wakomeshe vita hivi vya kikatili dhidi ya watoto Yemen”?
Amezitaka pande zote kinzani katika mzozo wa Yemen kuheshimu haki za kimataifa za binadamu zikiwemo za watoto. hii nikwamjibu wa radio ya umoja wa mataifa.

Post a Comment

0 Comments