Advertisement

Responsive Advertisement

Navigation Menu

Wanafunzi wa shule ya msingi AZIMIO iliopo manispaa ya morogoro wameiomba serikali iwakumbuke kutatua tatizo la ukosefu wa maji.
Wanafunzi wa shule ya msingi AZIMIO iliopo manispaa ya morogoro wameiomba serikali iwakumbuke kutatua tatizo la ukosefu wa maji linaloikabili shule hiyo kwa muda mlefu sasa.
    Wakizungumza na OKOA FM shuleni hapo baadhi ya wanafunzi wa darasa la saba REHEMA MUSSA na ABDALAH ATHUMANI wamesema ukosefu wa maji unaweza kusababisha kuenea kwa magonjwa ya mlipuko na vifo.
   Hatahivyo kwa upande wake mwalimu mkuu msaidizi wa shule ya msingi   AZIMIO, EDITH MKUDE amekili kuwepo kwa tatizo hilo la maji kwani ni muhimu kwa mkusanyiko wawatu wengi kama shuleni.
Aidha mwalimu wa taaluma ABEID NAMKAPE amesema adha hiyo  ya maji inasababisha kushuka kwa taaluma ya wanafunzi kwenye masomo yao kwani huchukuwa muda mrefu kutafuta maji kwenye makorongo yalio mbali na shule hiyo.
   Kwa mujibu wa shirika la umoja wa mataifa takwimu iliyotolewa mwishoni mwa mwezi huu, asilimia 69 ya shule kote Duniani hazina maji  safi ya kunywa na usafi wa vyoo bora.

Post a Comment

0 Comments