Advertisement

Responsive Advertisement

Navigation Menu

Wazee walivyo amua kufundisha hadithi kwenye vituo vyakulelea watoto yatima mkoani morogoro.


  Hadithi nimoja ya mafunzo makubwa  yanayotolewa  kwa  watoto wadogo kuanzia umli wa mwaka mmoja hadi miaka 20 kwakiasi kikubwa lengokuu la hadithi nikuendeleza  elimu , kuongeza maarifa , na upambanuzi wa mambo mengi ya dunia.
  Veronica Kapaya yeye ni bibi mwenye umli zaidi yamiaka  70 amesema  hadithi nikitu cha msingi sana kwajamii, zamani wakati wautoto wao mafundisho mengi waliyapata kupitia hadithi walizo simuliwa na bibi,babu na wazazi wao lakini kwasasa watoto na vijana wengi wao hawako tayali kukaa nakusikiliza hadithi hizo.
   Tanzaniakidstime ilifanikiwa kutembelea kituo cha kulelea watoto na wazee wasio jiweza kilichopo Changalawe mzumbe wilayani mvomero mkoa wa morogoro kinacho milikiwa na shirika lisilo la kiserikali Childhood Development Organisation na kufanya mahojiano na walimu ambao ni wazee wanaowafundisha watoto hadithi za zamani kilasiku ya ijumaa.
  Aidha bi, Mwajuma Saidi alisimulia hadithi inayo zungumzia wizi ambayo fundisho lake nikuwakanya watoto kuacha kutamani vitu visivyo halali yao kwani nidhambi mbele za mungu na nikinyume cha sheria, mazara yake nikupata Ulemavu, kuuwawa au kifungo cha maisha.
  Hata hivyo Asha Boko nimwanafunzi wa chekechea alisema anapenda na anafurahishwa na hadithihizo zinazo simuliwa hapo shuleni.

Post a Comment

0 Comments