Advertisement

Responsive Advertisement

Navigation Menu

Umaskini miongoni mwa watoto wamulikwa Uganda walio katika familia masikini:

Mkutano wa siku tatu unaonagazia hatima ya watoto walio maskini zaidi barani Afrika umeng’oa nanga hii  leo katika mji mkuu wa Uganda Kampala.
  Mkutano huo umewaleta pamoja watalamu 50 kutoka sehemu mbalimbali duniani kwa ajili ya kudurusu hatua na mikakati ambayo imekuwa na manufaa makubwa kusaidia watoto walio maskini zaidi barani Africa.
Kwenye ufunguzi wa mkutano huo, Dr. Doreen Mulenga, Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Matifa la Kuhudumia watoto, UNICEF, Uganda alionyesha matumaini kuwa mkutano huo utaweka bayana hatua muhimu ambazo zitaleta nuru katika maisha ya watoto waliomaskini Zaidi barani Africa.
 Akiongeza kwamba watahakikisha mifano ya mikakati muhimu itakayobainishwa inatekelezwa nchini Uganda ambako asilimia 55 ya watoto walio chini ya umri wa miaka 5 wanaishi katika umaskini wa aina tofauti huku wakinyimwa huduma na haki za msingi mathalani afya, elimu maji, usafi na malazi.
  Dr. Mulenga alibainisha kwamba ukosefu huo huwatia hatarini kunyanyaswa,  na kuathiri vibaya mustakbali wao.
UNICEF imeandaa mkutano huo katika ushirikiano na Kituo cha Utafiti wa Sera ya Kiuchumi (EPRC). Mkurugenzi Mtendaji wa, EPRC, Dr. Sarah Ssewanyana anatumai kuwa mkutano huu utasaidia watunga sera kuhakikisha kwamba watoto waliomaskini zadi wameondolewa kutoka umaskini huo na athari zake.
 Taarifa hii nikwa mjibu wa radio ya umoja wa mataifa.

Post a Comment

1 Comments

  1. I think this is an informative post and it is very useful and knowledgeable. therefore, I would like to thank you for the efforts you have made in writing this article. KIU

    ReplyDelete