Wizara ya afya maendeleo ya jamii jinsia wazee na watoto yatoa tahadhari dhidi ya bacteria hatari.
Bacteria hao nihatari kwenye mwili ambao husababisha uzalishaji wa kemikali hatari ambazo husababisha kuumwa sana na wakati mwingine hufikia hatua ya kupata mshituko.
SEPSIS inaweza husababishwa na maambukizi kwenye maeneo kamavile:-
-Mapafu
-Tumbo
-Figo
-Damu
DALILI ZA SEPSIS NIPAMOJA NA :-
-Homa Kali
-Mapigo ya moyo kwenda kwa haraka kuliko kawaida.
-Kupumua kwa haraka haraka
-Kupungua kwa mkojo
-Kupungua kwa uwezo wa akili
-Kupoteza fahamu
_Kudumisha usafi wa mwili ikiwa nipamoja na kunawa mikono Mara kwa Mara na kutunza vidonda katika hali ya usafi.
_Kwenda kwenye kituo cha huduma za afya mapema pindi unapo pata homa au unapo kua na kidonda.
_Kutumia dawa za antibiotiki kulingana na ushauri wa mtoa huduma za afya.
_Kuhakikisha watoto wanapata chanjo kulingana na ratiba ya chanjo.
0 comments:
Post a Comment