Advertisement

Responsive Advertisement

Navigation Menu

ZAIDI YA WATOTO TISINI WAFARIKI DUNIA DRC KWA TATIO LA UTAPIA MLO TANGU SEPTEMBA 1 MWAKA HUU.
 Kwa mujibu wa Takwimu   zilizotolewa na POP SECURITY, shirika la kijamii linalo pambana  dhidi ya tatizo la utapiamlo nchini DRC. jumla ya Watoto tisini na tano walio chini ya umri wa miaka 5, walifariki dunia kutokana na tatizo hilo tangu Septemba 1 hadi  Novemba 15 mwaka huu katika mji wa KIKWIT.

Aidha Vifo hivi vilijumuisha pamoja na  watoto wakimbizi walioko ndani ya mji huo wa KIKWIT katika mkoa wa KWILU, ambapo Zaidi ya asilimia arobaini hadi arobaini na tano wameathirika na ugojwa huo kama alivyo bainisha   Dr,PIERRE MANGEZI,   na kuongeza kwamba tatizo hilo ni sugu ndani ya mkoa wa  Kwango.

Takwimu hizi ziliwasilishwa na shirika hilo la POP SECURITY, mbele ya wakuu na viongozi wa  UNICEF  huko KINSHASA,  BUREAU ya mashariki,  Novemba 12 mwaka huu. Walipo fika KIKWIT, UNICEF ili jionea mtoto mmoja wa mwaka mmoja akilia katika mikono ya mama yake, kwa ukosefu wa chakula, na mtoto huyo alikuwa nautapimlo katika kituo cha afya cha MASANGO mkoani KWILU.

"Tunateseka, kuna hata watoto wetu ambao walikufa hapa, tunawaweka katika masanduku za carton na kuwazika. Hakuna msaada, "Alilia mzazi mmoja. Mbali Zaidi ni kwamba kila siku mtoto mmoja ana fariki katika hospitali hio kwa ugojwa huo wa utapia mlo”
aliongeza Dr.Pierre.
                                    
Hata hivyo  Baadhi ya Raia wa eneo hilo waliomba msaada kutoka shirika la UNICEF, lengo kuu likiwa ni kuokoa maisha ya watoto wao, ambao ni taifa la kesho, huku Msaada mkubwa ukiwa ni kuwatafutia Amani ili waweze kujilimia mashamba yao wenyewe.

Post a Comment

0 Comments