Advertisement

Responsive Advertisement

Navigation Menu

UMOJA WA MATAIFA NA UNICEF WALAANI MAUAJI YA WATOTO MKOANI NJOMBE:


                                          NJOMBE.
  Ofisi ya  Umoja wa Mataifa nchini Tanzania imetoa rambirambi yake kwa familia na jamii mkoani njombe kwa watoto ambao wameuwawa kikatili wiki chache zilizopita.

    Hayo yamesemwa na Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa BW. Alvaro Rodriguez January 29 mwakahuu jijini Dar es salam, mashambulizi na mauaji ya watoto haikubaliki,Watoto wana haki ya msingi ya kuwa salama na kulindwa dhidi ya ukatili ili waweze kufurahia utoto wao na kufikia kilele cha uhai wao.

  Aidha Umoja wa Mataifa inajiunga na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kulaani vitendo hivyo , “Sisi Umoja wa Mataifa tupotayari kusaidia Serikali katika juhudi zao za kushughulikia suala hilo, "alisema Bw Alvaro Rodriguez,. "Zaidi ya hayo, tunatoa wito kwa wadau wote kuungana pamoja kuhakikisha kwamba nyumba, shule na jamii ni salama kwa ajili ya watoto.
  
 Hata hivyo Mwakilishi wa UNICEF nchini Tanzania Bi Maniza Zaman, amesema."Aina ya unyanyasaji au matumizi mabaya dhidi ya mtoto haikubaliki na kitendo chochote kibaya ni ukiukwaji wa haki zao za msingi".

Post a Comment

0 Comments