Advertisement

Responsive Advertisement

Navigation Menu

UN RADIO YACHAPISHA TAARIFA IKISEMA zaidi ya watoto milioni 20 walizaliwa duniani kote wakiwa na uzito


  Idhaa ya Kiswahili ya Radio ya umoja wa Mataifa (UN RADIO) Ilichapisha taarifa za Takwimu mpya zilizotolewa na watafiti kutoka mashirika ya Umoja wa Mataifa na Chuo cha tiba za kitropiki na afya cha London, Uingereza zimeonyesha kuwa mwaka 2015 zaidi ya watoto milioni 20 walizaliwa duniani kote wakiwa na uzito wa chini kupindukia, ambao ni chini ya kilo mbili na nusu au pauni 5.5
Kiwango hicho ni mtoto 1 kati ya watoto 7 ambapo takribani asilimia 75 ya watoto hao walizaliwa katika nchi za Asia ya Kusini na zile za Afrika zilizo kusini mwa jangwa la Sahara.
Tatizo ni kubwa kwa nchi zilizoendelea pia
Hata hivyo watafiti hao wanaojumuisha wale wa shirika la afya duniani, WHO, shirika la kuhudumia watoto UNICEF na Chuo hicho Kikuu cha London, wamesema bado tatizo la watoto kuzaliwa na uzito mdogo ni la juu kwenye nchi za kipato  cha juu barani Ulaya, Amerika Kaskazini, Australia na New Zealand.
Wamesema katika maeneo hayo hakuna hatua madhubuti zimechukuliwa tangu mwaka 2000 kupunguza tatizo la watoto kuzaliwa na uzito mdogo, wakizingatia utafiti wao uliohusisha mataifa 148 na vizazi hai milioni 281,  utafiti ambao umechapishwa katika jarida la masuala ya afya la Lancet.
Hatua hizo hazijachukuliwa, ingawa kwamba mwaka 2012, mataifa yote 195 wanachama wa WHO waliazimia kupunguza kwa asilimia 30 idadi ya watoto wanaozaliwa na uzito mdogo ifikapo mwaka 2025 wakilinganisha na viwango vya mwaka 2012.

Post a Comment

0 Comments