Advertisement

Responsive Advertisement

Navigation Menu

Chonde chonde wazazi wetu changieni chakula iliwalimu waanze kutupikia hapashuleni,hayo nimaneno ya wanafunzi wa shule ya msingi USHOKOLA wilaya ya kaliua mkoani tabora wakiwaomba walimu na wazazi kuhusu chakula shuleni.      

  Wanafunzi katika shule ya msingi USHOKOLA wilaya ya KALIUA mkoani TABORA wamewaomba wazazi kuchangia chakula kwa ajili ya wanafunzi. Wakizungumza na TKT RADIO Wanafunzi wamesema kutokana na kukosekana kwa chakula shuleni hapo wamekuwa wakipata changamoto wakati wa vipindi ikiwa pamoja na kutokuelewa vizuri waalimu wanapofundisha.

    Mwalimu AMINA MKUMBO  ni mhasibu katika shule ya msingi USHOKOLA amesema mpango wa chakula haupo kwa sababu ya shule hiyo kukabiliwa na changamoto ya uhaba wa vyumba vya madarasa jambo linalosababisha wanafunzi kuingia kwa shifiti.
MKUMBO amewataka wazazi kujitokeza na kushiriki ujenzi wa miundombinu ya shule ambapo kwa sasa shule ina jumla ya vyumba kumi na mbili vya madarasa, Katika kutatua changamoto ya uhaba wa vyumba vya madarasa shuleni hapo afisa mtendaji wa kata ya USHOKOLA, MOHAMEDI MUSHI amesema wamekubaliana na wazazi kuanza mchango kwa ajili ya ujenzi.

  Kwa upande wao baadhi ya wazazi wamesema watashiriki kikamilifu kutoa mchango ili kuongeza vyumba vya madarasa shuleni hapo na kuanza kutoa chakula kwa wanafunzi. Na Simon Jumanne.

Post a Comment

1 Comments

  1. Wazazi na walezi bado tuna wajibu mkubwa wa kufanya hakika

    ReplyDelete