Advertisement

Responsive Advertisement

Navigation Menu

Halmashauri ya wilaya ya KALIUA mkoani TABORA imezindua mfuko wa elimu kama njia ya kuongeza ufaulu kwa wanafunzi wa shule za msingi na sekondari.


  Halmashauri ya wilaya ya KALIUA mkoani TABORA imezindua mfuko wa elimu kama njia ya kuongeza ufaulu kwa wanafunzi wa shule za msingi na sekondari.
  Uzinduzi huo wa mfuko wa elimu umefanyika kwenye kikao cha baraza la madiwani la halmashauri ya wilaya ambapo mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya KALIUA,      
Daktari JOHN PIMA amesema lengo la kuanzisha mfuko wa elimu ni kuhakikisha wilaya inaendelea kufanya vizuri kielimu.


 Daktari PIMA amesema halmashauri itatoa motisha kwa waalimu na wanafunzi watakaofanya vizuri kwenye mitihani yao.
Aidha jumla ya milioni kumi na mbili zimepatikana kwenye uzinduzi huo huku akitoa rai kwa wananchi kuwa na mwito wa kuunga mkono mfuko ulioanzishwa.
   
 Kwa upande wake mwenyekiti wa bodi ya kusimamia mfuko huo mchungaji AMOS CHIDEMI wa kanisa la Angilikana amesisitiza kuwepo kwa ushirikiano baina ya viongozi.
Na baadhi ya wanafunzi wamesema kuanzishwa kwa mfuko huo utakuwa chachu ya wao kusoma kwa bidii na kuendelea kufanya vizuri zaidi katika masomo yao. Imeandaliwa na mwandishi wentu Simon Jumanne kutoka Kaliua Tabora.


Post a Comment

0 Comments