Advertisement

Responsive Advertisement

Navigation Menu

Karagwe ya pata ufumbuzi wa tatizo la udumavu kwa watoto, kupitia kwenye vikundi vya wanawake.


 Karagwe.Wanawake wilayani karagwe mkoani Kagera kupitia katika vikundi vyao vya maendeleo wametakiwa kujikita katika utoaji wa elimu ya lishe ili kuwezesha wilaya hiyo na mkoa wa Kagera kwa ujumla kuondokana na udumavu kwa watoto.
 
    Akizungumuza na wanawake wa kikundi cha wanawake na maendeleo katika kata ya Kayanga wilayani Karagwe wakati wa zoezi la kuwajengea uwezo kuhusu njia za kujikomboa kiuchumi katibu wa mbunge wa jimbo la Karagwe Ivo Ndisanye amesema kwamba kutokana na wilaya Karagwe kuwa miongoni mwa wilaya zinazokabiliwa na hali ya udumavu kwa watoto ni vyema wanawake kupitia katika vikundi vyao vya maendeleo wakajikita katika utaoaji wa elimu ya kuhamasisha lishe nzuri hasa kwa watoto ili kusaidia wilaya Karagwe na mkoa Kagera kwa ujumla kuondokana na udumavu.
   Aidha wilaya Karagwe imeendelea kukabiliwa na hali ya udumavu kutokana na idadi kubwa ya familia kuendelea kula chakula cha aina moja, kuuza vyakula  vyenye lishe sokoni badala ya kuvitumia ni pamoja na baadhi ya wakina mama kutojali lishe kwa watoto wao na kujikita zaidi katika shughuli za ujasiriamali.

  Hata hivyo baadhi ya wanawake Jovitha Kombe diwani wa viti maalum tarafa Nyabiyonza na Doresela Reopord wamesema kuwa kutokana na elimu waliyopatiwa watasaidia vikundi vingine vya wakina mama kuvijengea uwezo wa kuedelea kuelimisha suala la lishe kwani bado mwitikio wa wakina mama wilayani Karagwe kuthamini suala la lishe kwa watoto hasa vijijini haujaridhisha.
 Na mwandishi wetu Jovinus Ezekieli kutoka Karagwe Kagera.

Post a Comment

0 Comments