Advertisement

Responsive Advertisement

Navigation Menu

Kutoka hospital ya wilaya ya kahama inasemekana kunyonyesha mtoto miezi sita (6) ya mwanzo mtoto hataweza kuugua mara kwa mara na huongeza upendo kwa wazazi wake.


   Afisa Muuguzi Katika Hospital ya wilaya ya Kahama Mkoani Shinyanga kitengo cha Uzazi Salama na Mtoto Bi,Joseline Jacob amesema jamii inatakiwa kujua umuhimu wa kunyonyesha watoto kwa kipindi cha miezi sita ya mwanzo bila kumpa kitu chochote kwani maziwa ya mama yana lishe tosha kwa mtoto na yanamkinga dhidi ya magonjwa mbalimbali.
    
  Bi,Jacob ameiambia TKT RADIO kwamba Mtoto akinyonya maziwa ya mama pekee yana umuhimu katika ukuaji wake wakilasiku na uimalishaji wa serizake za mwili,Aidha Mama anapokuwa ananyonyesha mtoto mara kwa mara inamsaidia mama huyo kutopata Ujauzito Mapema huku akitaja hasara zinazopatikana pindi Mtoto anaposhindwa kunyonya maziwa ya kutosha kutoka kwa Mama yake.
  Kwa upande wao Akina Mama wanaonyonyesha Bi,Ester Edward na Halima Magodoro wamesema zipo faida nyingi kwani inaongeza upendo kati ya Mtoto na Mama, Vile vile hataweza kuugua mara kwa mara.Na Joseph Sepetu, Kahama Shinyanga.


Post a Comment

1 Comments

  1. The easygoing equestrian rigging could be riding breeches coordinated with a plain shirt. dailytramadol.com website

    ReplyDelete