Advertisement

Responsive Advertisement

Navigation Menu

Mbali na mauwaji ya watoto, kesi 64 zimeripotiwa za ukatili dhidi ya watoto wilaya ya ludewa mkoani njombe tangu mwezi jannuary 01 hadi junne 30 mwakahuu.LUDEWA NJOMBE: Picha ni kwamsaada wa Morondiokwetu blog.

 Kutokana na Matukio mbalimbali ya ukatiri kwa watoto hapa nchini  Serikali kupitia idara ya ustawi wa jamii wilayani Ludewa Mkoani  Njombe imetakiwa kutoa Elimu ya ukatiri kwa jamii ili jamii iweze  kuachana na vitendo vya ukatiri kwa Watoto.
 RAHI hiyo imetolewa na Imamu wa Msikiti Mkuu wa Wilaya ya Ludewa  Imamu Haruna Rahimu alipokuwa anazungumzia suala la ukatiri kwa  watoto ambapo amesema jukumu la kumlinda Mtoto linaanza katika  ngazi ya familia,Jamii na serikali.

AMESEMA mara nyingi ukatiri unaotokea katika jamii unatokana na  jamii kutopata elimu yakutosha yakujua ni kwanini wanafanya  ukatiri kwa watoto kwani ukatiri umegawanyika katika makundi.

AMESEMA" suala la ukatiri kwa watoto linategemeana,kwani mtoto  anaweza kufanyiwa ukatiri kutoka kwa jamii au wazazi na walezi  ambao mtoto amekuwa anaishi nao" amesema Rahimu
NAO baadhi ya  wanafunzi wa shule za sekondari Wilayani Ludewa  wameishauli Jamii kuachana na vitendo vya ukatiri sambamba na  kuiasa serikali kutoa adhabu kari kwa mtu yoyote atakaye sadikika  amemfanyia ukatiri  mtoto.

Hatahivyo kinachotakiwa kwa jamii ni kubadilika kutokana na mfumo  wa maisha ya sasa,kwani mtoto ndiye taifa la kesho kwaiyo  akifanyiwa ukatiri si jambo zuri kwaiyo serikali inatakiwa  kuingilia kati na jamii inatakiwa kujitambua.
 
 Chiwango amesema wamepokea kesi nyingi za ukatiri kwa watoto,kesi  hizo ni zawatoto kutelekezwa ukiachilia mbali kesi za watoto  kuuliwa sio nyingi sana katika Wilaya ya Ludewa Na, Salum Mohamed

Post a Comment

2 Comments

  1. Asante kwa taarifa hiyo ,nafikiri jamii nzima tunawajibika katika hili ili kupunguza kama siyo kutokomeza kabiza ukatili kwa WATOTO.

    ReplyDelete
  2. Asante kwa taarifa hiyo ,nafikiri jamii nzima tunawajibika katika hili ili kupunguza kama siyo kutokomeza kabiza ukatili kwa WATOTO.

    ReplyDelete