Advertisement

Responsive Advertisement

Navigation Menu

TAULO ZA KIKE KUMBE ZINAWEZA KUWA TIBA YA KUUDHULIA NA KUONGEZA UFAURU WA MASOMO KWA WATOTO WAKIKE SHULE ZA MSINGI NA SEKONDARI?VIONGOZI WA WILAYA YA KALIUA MKOANI TABORA WAMEANZA UTAFITI HUO WAKISHIRIKIANA NA WAZAZI.Wanafunzi wa kike katika shule za msingi na sekondari katika kata ya UFUKUTWA wilaya ya KALIUA mkoani TABORA wameiomba serikali kupitia wizara ya elimu kutenga bajeti ya kununua na kuzigawa mashuleni taulo za kujisitili wakati wa hedhi ili kuinua taaluma kwa mtoto wa kike, Wakizungumza kwenye kikao kilichowakutanisha wazazi wa kike pamoja na wanafunzi wa kike wa shule ya sekondari UFUKUTWA na shule zote za msingi katika kata ya UFUKUTWA baadhi ya wanafunzi wameeleza adha wanazozipata wakati wa hedhi ikiwa pamoja na kukosa baadhi ya vipindi darasani hali inayopelekea kushuka kitaaluma.

  Kutokana na changamoto hizo wameiomba serikali kuweka mkakati wa kusambaza taulo hizo katika shule za msingi na sekondari, ilikuendelea kuwasaidia mabinti hao, Madamu SANGA ni mwalimu wa malezi shule ya sekondari KAPUYA amewataka wazazi wa kike kuwa karibu na watoto wao hasa wanapokuwa katika mzunguko wa hedhi waweze kuwasaidia mengi yanayo wasibu, Hatahivyo  afisa mtendaji wa kata ya UFUKUTWA, HAPPINESS  MASENGWA amesema kwa kushirikiana na wazazi wamekubaliana kutoa shilingi elfu moja kwa kila mzazi mwenye mtoto kwa ajili ya kununua taulo za kike.
  Nao baadhi ya wazazi wamesema wataweka hamasa ili kufanikisha makubaliano ya mchango huo,Katika kikao hicho wanafunzi wamepata elimu ya athari za mimba za utotoni na namna ya kuboresha elimu kwa mtoto wa kike ambapo waelimishaji mbali mbali wakiwemo dawati la jinsia wilaya ya KALIUA, Afis a usitawi wa jamii na viongozi wengine wa serikali wamepata wasaa wa kutoa maada zao. Na Simon Jumanne kutoka KALIUA mkoani TABORA.

Post a Comment

0 Comments